top of page

Faith Group

Public·70 members

Ashot Agafonov
Ashot Agafonov

Kilimo Cha Maharage Pdf ((FREE)) Download


Palizi ya kwanza inaweza kufanyika Kati ya siku 8-12 baada ya mmea kuota na palizi ya pili ifanyike siku ya 20- 30 baada ya palizi ya kwanza. Kufanya hivi husaidia kuyalinda maua ya maharage yako yasipukutike wakati wa palizi hakikisha unaepuka palizi kipindi cha uwekaji maua.




kilimo cha maharage pdf download



Funza wa maharage ni wadudu wanaoshambulia mimea michanga ya maharage. Funza wa maharage hawa huweza kusababisha uharibifu hadi kufikia asilimia 100 kufuatana na hali ya hewa-unyevu kidogo, rutuba kidogo, kuwepo kwa maotea ya aina ya maharage na magonjwa kwenye udongo, kurudia kupanda zao la maharage kila msimu na aina ya maharage.


Magonjwa maarufu ni adui katika ukuaji maharage, madoa pembe, kutu, magonjwa yanayosababishwa na bacteria na virusi. Mbegu iliyoambukizwa, udongo na takataka za maharage ni vyanzo vikubwa vya uambukizaji kwa magonjwa yote isipokuwa ugonjwa wa kutu ya majani.


Maharage ni zao maarufu zaidi duniani kati ya mazao mengine ya jamii ya mikunde. Maharage yalifika Tanzania miaka mia tatu (300) iliyopita. Nchini Tanzania na sehemu kubwa ya Afrika Mashariki, maharage yanazalishwa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na kwa ajili ya kuuza. Wakulima wa Afrika mashariki wanazalisha zaidi ya nusu ya maharage yanayozalishwa barani Afrika. Nchini Tanzania, mara nyingi maharage yanapandwa pamoja na mahindi au na zao la kudumu kama ndizi au kahawa.


Kati ya robo moja hadi theluthi moja za kaya wanauza maharage, na yanauzika kirahisi Tanzania na nchi za jirani. Wenye mapato madogo mjini na asilimia themanini (80%) ya Watanzania waishio vijijini wanaotegemea kilimo, wanakula haya maharage yenye protini na vitamini kila siku.


Palilia ukiondoa magugu makubwa. Fukia magugu madogo ili kuongeza viumbe hai kwenye udongo. Vunja udongo ulioshikana hasa kwenye mstari wa kupanda. Mistari ya mwinuko au matuta yanafaa zaidi kwaajili ya kupanda maharage haya. Shamba lililo andaliwa vizuri maharage huota mapema na huweza kupunguza matatizo ya magugu kuwa mengi, wadudu, na magonjwa shamabani.


Nchini Tanzania, yafuatayo hapo chini ni aina ya maharage ambayo yanastahimili magonjwa sugu ya maharage kama chule, bakapembe, kutu ya majani, kuvu nyeupe, uozo wa mizizi, bakajani na batobato maharage:


Wakulima wanatakiwa kuchagua aina ya maharage ambayo tayari yana masoko na, yanakidhi matarajio ya familia kiladha na kimapishi. Kuchagua aina ya maharage, utahitaji utafiti wa mkulima au vikundi vya wakulima kwenye soko.


Kwenye udongo usio na rutuba, ni muhimu kuongeza kirutubisho cha nitrojeni kwa ajili ya kukuza maharage. Wakulima wanaweza kutumia mbolea za kupandia kama DAP, Minjingu mazao, au Yara Legume. Hauhitaji vitu vingine vyakuongezea. Tahadhari kwamba, naitrojeni inaongeza ukuaji wa majani, na ukizidisha, itasababisha kuwa na mimea mikubwa lakini mavuno machache.


Kagua shamba lako mara kwa mara kuwachunguza wadudu ambao wanaweza kuathiri maharage yako shamabani. Wadudu wanao athiri sana maharage nchini Tanzania ni kama vile, funza, buu/ funza inzi maharage, funza wa miche ya maharage, inzi mweupe, vidukuri, mbawa kavu wa majani, mbawakavu wa maua na, funza wa vitumba vya maharage na wadudud wanaofyonza mifuko ya maharage.


Katika sehemu kubwa ya ardhi zinazozalisha maharage Africa, kuna mapungufu ya madini ya fosiforusi kwa matumizi ya mimea. Pia kuna upungufu wa unyevu nyevu kwenye ardhi. Vitu hivi viwili vinaweza kupunguza mavuno ya maharage. 350c69d7ab


About

Welcome to the group! You can connect with other members, ge...

Members

  • Nirvana yoga school India
    Nirvana yoga school India
  • Table Tennis
    Table Tennis
  • Maverick Wright
    Maverick Wright
  • arqammehboobskp1
  • Shirley Price
    Shirley Price
bottom of page